suivre
Jumanne, 16 Septemba 2014 00:00

Rajua Featured

Written by

Afrocentricity International inasaidia kuinua uchumi, utamaduni na elimu ya Mwafrika katika jitihada za kujenga urazini wa kiutamaduni. Mkabala wake umekitwa katika Uafrika na Umajumui wa Kiafrika, ikishiriki katika ngazi ya kitaifa na kimataifa kuandaa kundi la watu wenye ujuzi wa hali ya juu wenye lengo la kuleta mvuvumko wa Kiafrika. Kundi hili linasaidia kuandaa nafasi kwa ajili ya ujenzi wa kanzi za data, vikundi vya kusaidiana, na waibuzi mahiri wa maarifa mapya ambao wataimarisha vuguvugu la kumwinua Mwafrika na kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa ya Afrika. Dhamira kuu ya vuguvugu hili, tangu kuasisiwa na kuundwa kwake katika duru, mikondo, vilabu, vikundi na asasi mbalimbali za Uafrika duniani, ni kuwa na sauti moja ya Afrika inayotokana na uzoefu wa idadi kubwa ya watu wetu ili kufanikisha malengo yetu ya kurejesha utu wetu kama tulivyofanikiwa kurejesha ardhi zetu, ili kuendeleza uhuishaji wa tamaduni za Mwafrika mahali popote duniani, na kumahiria maarifa ambayo yaliasisiwa, na kudumishwa na wahenga. Katika kutekeleza dhamira yetu, tunathamini mchango wa wapigania uhuru wetu, magwiji waliotupatia lugha na mikakati ya ushindi, na harakati muhimu za kujenga uchumi imara na mahusiano madhubuti ya kijamii miongoni mwa Waafrika. Sisi si tu chemchemi ya taarifa, bali pia ni vuguvugu hai, imara, na la kisasa linalolenga kulinda maslahi ya Mwafrika na kudumisha manufaa tuliyokwishafanikisha duniani. Maisha yetu yanahusiana, na malengo yetu ni ya kimataifa na tunaongozwa na historia ya waliojitoa muhanga kwa ajili ya ushindi dhidi ya vikwazo vyote. Tunakusudia kufanikiwa, ukanda mmoja baada ya mwingine, jiji moja baada ya jingine, na kitongoji kimoja baada ya kingine.


Dkt. Ama Mazama, Per-aa-Kimataifa
Dkt. Molefi Kete Asante, Mwakilishi-Kimataifa

 

{youtube}Wyv1XRKkx2s{/youtube}

Read 7256 times Last modified on Alhamisi, 18 Septemba 2014 01:23

Login